Msajili wa Hazina ateta na Menejimenti ya HESLB

DAR ES SALAAM-Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amekutana na kuzungumza na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Dkt. Bill Kiwia.
Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Bill Kiwia (wa pili kushoto), katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimefanyika Aprili 25, 2024 katika Ofisi za Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujitambulisha kwa Menejimenti hiyo, kufuatia uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa HESLB.
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dkt. Bill Kiwia (kushoto), akizungumza alipokuwa akitoa wasilisho lake kwa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu (kulia), katika kikao hicho.

Katika kikao hicho, viongozi hao wawili walijadiliana masuala mbalimbali yanayolenga kuongeza ufanisi na tija kwa kuzingatia falsafa ya R4 ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu (kushoto), akiagana na mgeni wake Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia (kulia), mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, katika kikao kilichofanyika Dar es Salaam.
Aidha, katika kikao hicho Dkt.Kiwia akiwasilisha mikakati yake itakayowezesha taasisi hiyo kufikia malengo yake ya kuhakikisha vijana wengi wa kitanzania wanatimiza ndoto zao za kusoma elimu ya juu, kwa kunufaika na mikopo wanayoitoa kwa manufaa ya jamii zao na Taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news