Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang jela miaka 20 kwa ubadhirifu

MANYARA-Mahakama ya Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara imemhukumu aliyekuwa mkusanya mapato kwa kutumia mashine ya POS wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Bw. Petro Michael Muray.
Mshitakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la ubadhirifu, kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2022.

Hukumu hiyo dhidi ya Bw. Petro Michael Muray katika shauri la Uhujumu Uchumi Na.03/2023, imetolewa Aprili 19,2024 na Mhe. Anorld Kileo - Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hanang'.

Mshtakiwa ameamriwa kwenda jela miaka 20 na ametakiwa kurejesha kiasi cha shilingi 3,532,000.

Mshitakiwa alifanya ubadhirifu wa fedha hizo kupitia makusanyo ya fedha kwa njia ya POS ambapo alikuwa akikusanya fedha zilizotokana na vyanzo vya misitu Wilaya ya Hanang'.

Mshitakiwa amepelekwa magereza kutumikia kifungo chake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news