Rais Dkt.Mwinyi awashukuru wananchi, viongozi kwa kuendelea kumuombea dua njema hayati Ali Hassan Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa shukrani zake za dhati kwa wananchi na viongozi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kuendelea kumuombea dua na hitma baba yake mzazi hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na viongozi na wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili mstaafu Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi,ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh,Saleh Omar Kabi (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Hadid Rashid Hadid, iliyofanyila leo 12-4-2024 katika Masjid Hidaya Kilimani Tazari Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu).

Alhajj Dkt. Mwinyi, ametoa shukurani hizo mara baada ya ibada ya sala ya Ijumaa iliyofuatiwa na visomo mbalimbali, hitma na du’a kweye masjid Hidaya, Kilimani Tazari, Mkoani humo.
Akizungumza kwa niaba ya familia yake, Alhajj Dkt. Mwinyi amewashukuru wananchi hao kwa mapenzi yao kwa Mzee Mwinyi tangu walipomuuguza hadi alipokufa Februari 29 mwaka huu.

Naye, Mkuu wa Mkoa huo, Rashid Hadid Rashid alisema wanachi wa Kijiji cha Kilimani Tazari na vijiji jirani, kwa makusudi waliamua kukaa pamoja kumuombea dua Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi, viongozi waliopo hai na wazee wa vijiji hivyo waliofariki duni.
Akizungumza kwenye ibada hiyo, Sheikh Khamis Abdul Hamid aliwahusia waumini wa kiislam kuendelea kufanya mema na kumcha Mwenyezi Mungu kwa haki ili roho zao zikawekwe mahala pema baada ya kufa.

Mapema akikhutubu kabla ya sala ya Ijumaa, Khatib Sheikh, Omar Abdi aliwasihi wananchi na waumini wa dini ya Kiislam kuendelea kujenga hofu kwa Mwenyezi Mungu kwa kukithirisha ibada hata baada ya kumalizika kwa Mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Aliusia kwamba Mwenyezi Mungu hayupo Mwezi wa Ramadhan pekee bali yupo siku zote, hivyo aliwanasihi waumini hao, kuendeleza ibada kwa siku za kawaida kama ilivyokuwa Ramadhan.

Ibada hizo za visomo na du’a na hitma pia waliombewa viongozi waliopo serikalini, wastaafu, masheikh na wazee walio hai na waliotangulia mbele ya haki ndani na nje ya Mkoa huo.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali akiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh, Saleh Omar Kaab, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Rashid Hadid na viongozi wengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news