Rais Dkt.Samia apokea ripoti ya maafa ya mafuriko nchini

ZANZIBAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameongoza kikao maalum kilichowasilisha ripoti ya maafa ya Mafuriko yaliotokea sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Rufiji, Morogoro, Lindi na Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akiwasilisha ripoti ya maafa ya Mafuriko yaliotokea sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Rufiji, Morogoro, Lindi na Arusha, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 13, Aprili 2024.

Vile vile, kamati maalum imewasilisha maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 13, Aprili 2024.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa kikao maalum kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kilichowasilisha ripoti ya maafa ya Mafuriko yaliotokea sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Rufiji, Morogoro, Lindi na Arusha pamoja na maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 13, Aprili 2024.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria kikao maalum kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kilichowasilisha ripoti ya maafa ya Mafuriko yaliotokea sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Rufiji, Morogoro, Lindi na Arusha pamoja na wasilisho la Kamati Maalum juu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 13, Aprili 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news