Rais wa IPU, Spika Dkt.Tulia ateta na Balozi wa Norway nchini

DODOMA-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tine Tonnes Ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma leo tarehe 24 Aprili, 2024.
Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Norway amemshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ziara aliyoifanya hivi karibuni nchini humo ambapo amesisitiza kuwa imeongeza chachu ya mashirikiano ya kidiplomasia sambamba na kukuza jitihada za uwekezaji kwenye maeneo ya kilimo, nishati mbadala, elimu na jitihada za kusaidia miradi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi na athari zake.
Kwa upande mwingine, Dkt.Tulia ameishukuru Serikali ya Norway kwa kuendeleza mashirikiano mazuri na Tanzania hususani juu ya miradi wanayoendelea kufadhili nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news