RC Chalamila awatoa hofu wananchi uharibifu wa barabara, asema mambo mazuri yanakuja Dar

DAR ES SALAAM-Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mheshimiwa Albert Chalamila amesema, mvua nyingi zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa zimepelekea uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara, lakini Serikali haijalala iko imara.
Amesema, hivi karibuni miundombinu hiyo itarekebishwa na kujengwa barabara kwa kiwango cha lami.

RC Chalamila ameyasema hayo leo Aprili 15,2024 wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala Boma.

Amesema, katika mkoa huo kila wilaya barabara zitajengwa ikiwemo Ilala kilomita 55.27, Ubungo Km 54.27, Kigamboni Km 42.11, Temeke Km 52.71 na Kinondoni Km 48.33.

Pia, ametoa rai kwa wakandarasi wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi nzuri waombe kazi hiyo mara tu itakapotangazwa.

Aidha,RC Chalamila amesema,Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anadhamira ya dhati katika kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi katika nyanja anuai, hivyo amewaomba wananchi kuwa watulivu kutokana na kadhia wanayoipata ambayo imesababishwa na uhalibifu wa barabara katika maeneo yao kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news