Ujumbe kutoka Umoja wa Uwazi na Uwajibikaji (EITI) wakutana na kampuni za madini na gesi

DAR ES SALAAM-Ujumbe kutoka Asasi ya Umoja wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (EITI) ukiongozwa Katibu Mtendaji Bw. Mark Robinson na umekutana na wawakilishi wa Kampuni za Madini na Gesi na mashirika ya Umma ya TPDC na Stamico kujadili utekelezaji wa shughuli za EITI nchini.
Maeneo yaliyolengwa katika majadiliano hayo ni ushiriki wa kampuni na mashirika ya Umma (State Owned Enterprises -SOEs) yanayofanya shughuli za Uziduaji katika utekelezaji wa vigezo vya Kimataifa vya Uwazi na Uwajibikaji vya mwaka 2023 ( EITI Standard 2023) Aprili 4, 2024 jijini Dar es Salaam.

Mapitio ya matokeo ya Tathmini (Validation) ya mwaka 2023 ambapo masuala yafuatayo yalipendekezwa kuboreshwa ili Tanzania ifanye vizuri katika Tathmini ijayo ya mwaka 2027, uwekaji wazi wa mikataba ya Madini na Gesi Asilia na uwekaji wazi wa Wamiliki wanufaika (Beneficial Owners) katika kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia.
Mchango wa wachimbaji wadogo na urasimishaji wa sekta ya uchimbaji mdogo.

Ushiriki wa kampuni na SOEs katika utekelezaji wa vigezo vipya vilivyoongezwa (EITI Standard 2023).

Vigezo hivyo ni pamoja na masuala ya kuzuia rusha, jinsia na mazingira na Energy Transition.
Aidha, katika majadiliano hayo, ilielezwa kuwa baadhi ya kampuni tayari zimeweka wazi mikataba yake kupitia masoko ya hisa na hivyo iko wazi kwa Umma pia ilielezwa kuwa uwekaji wazi tayari mikataba utasaidia kuhamasisha Uwazi na wananchi kujua faida kutoka katika uvunaji wa rasilimali madini Mafuta na Gesi.

Wawakilishi watatoa ushirikiano kwa Sekretariati ya EITI Tanzania katika utekelezaji wa vigezo vya Kimataifa vya mwaka 2023.






Pia, Wawakilishi wa kampuni na mashirika yafuatayo walihudhuria. Pan Africa Energy, Maurel & Prom, Tanzania Chamber of Mines, Tembo Nickel, Shanta Gold Mine, TPDC na Stamico.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news