Wakili, mfanyabiashara Dar washtakiwa kwa kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo

DAR ES SALAAM-Leo Aprili 25, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Ilala mkoani Dar es Salaam limefunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi namba 10936/202
Picha haina uhusiano na watuhumiwa husika

Ni mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,Mhe. Rehema Lyana ambapo washtakiwa ni David Andindilile ambaye ni Wakili wa kujitegemea, na Hamza Suleiman Rajabu ambaye ni mfanyabiashara.

Kwa pamoja wamesomewa jumla ya mashtaka 14 ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na utakatishaji fedha haramu.

Makosa hayo ni kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16 marejeo ya 2023 pamoja na Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha Sura 423 marejeo ya 2023.

Washtakiwa hao wamekana makosa yao na kupelekwa mahabusu kutokana na kukosa vigezo vya dhamana.

Aidha,mshtakiwa Daniel Stanford Semwenda katika kesi hiyo, hakusomewa mashtaka yake kwa kuwa anaishi nje ya nchi na juhudi za kumtafuta ili ashtakiwe zinzinaendele.

Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 9, 2024 kwa ajili ya hoja za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news