Wananchi wajichotea maarifa banda la BoT katika Maonesho ya Biashara ya Miaka 60 ya Muungano


Wataalamu kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakitoa elimu kuhusu majukumu ya msingi ya BoT kwa wananchi wanaotembelea banda letu kwenye Maonesho ya Biashara ya Miaka 60 ya Muungano yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Jukumu la msingi la Benki Kuu ya Tanzania ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.
Majukumu mengine ya Benki Kuu ya Tanzania ni kutoa sarafu ya nchi ambayo ni Shilingi ya Tanzania,kusimamia na kudhibiti mabenki na taasisi za fedha, kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo nchini.
Pia, kuhifadhi akiba ya nchi ikiwemo fedha za kigeni,Benki ya Serikali, Benki ya Mabenki na
kutoa ushauri juu ya masuala ya uchumi na fedha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news