Waziri Mhagama awataka wananchi kuondoka maeneo hatarishi

MOROGORO-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amewataka wananchi kuondoka katika maeneo hatarishi ili kujikinga na mafurikio ya mvua za vuli zinazoendelea kunyesha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akizungumza na kuwafariji wananchi waliokumbwa na maafa ya mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro.

Kauli hiyo ameitoa Aprili 11,2024 wakati alipotembelea na kujionea maeneo yaliyokubwa na mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya ya Mlimba mkoani Morogroro ambapo amewaomba wananchi kuendelea kufuatilia na kusikiliza ushauri wa serikali.

"Niwaombe wananchi tuendelee kushikamana ili kupambana na majanga ya mvua na Mafuriko, ambayo yameleta kadhia kubwa sana kwa wananchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na viongozi wengine kabla ya kuanza safari ya kuwatembelea na kuwafariji wananchi waliokumbwa na mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro.

“Serikali imetengeneza Mpango wa Dharura wa kukabiliana na mvua za El Nino na mvua za Masika, ambapo serikali itafanya kila linalowezekana kuzuia madhara yasitokee na hasa maisha ya watanzania,” amesema Waziri Mhagama.

Ameongeza kuwa,mafuriko ya maji yamesababisha udongo kumomonyoka na kuharibu miundo mbinu ya reli na kuleta madhara mengine mengi niwaombe wanamlimba tuendelee kuangalia na kusikiliza ushauri wa serikali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi maalumu Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima walipotembelea na kuwafariji wananchi waliokumbwa na maafa ya mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya Mlimba Mkoani Morogoro.

“Serikali itaendelea kuhakikisha inapambana dhidi ya magonjwa ya Mlipuko na uhaba wa chakula na madhara mengine ambayo yameathiri wananchi, serikali itakuwa pamoja na nyinyi katika kutatua kadhia hizo alibainisha,” Waziri Mhagama

Niwaombe wananchi tuendelee kumuomba wenyezi Mungu hali iliyopo mbele yetu iweze kupita kwa haraka na ipite kwa usalama mkubwa.
Timu ya wataalamu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) sambamba na timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya wakiwa katika usafiri wa kiberenge kulekea eneo liloathirika na mafuriko ya maji na mvua Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro.

Ameeleza kwamba katika utabiri wa hali ya hewa unaoendelea kutolewa unaonesha mvua hizi zinaendelea kunyesha hivyo ni vyema tukaendelea kujichukulia tahadhari sisi wenyewe.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kilombero Mhe. Dustan Kyobya amesema changamaoto ya Mawasiliano ya barabara kwa watu wa Masagati na Utengule kwao wamekuwa kisiwa kutokana na miundo mbinu ya barabara kutopitika, lakini pia Mawasiliano kati ya Jimbo la Ifakara na Mlimba ambazo zinatengeneza wilaya ya kilombero nayo ni magumu.
Matukio katika ni muonekano wa juu kwa baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya Mlimba.

Aidha,miundombinu ya reli ilidondokewa na udongo na kusababisha kukatika kwa makalvati ya reli hivyo kusababisha usafiri wa kutoka Mlimba kuelekea makambako kutokuwepo.

“Nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuma ndege kwa ajili ya kuokoa watu waliokwama na kuruhusu treni ya Mwakyembe kuanza kubeba abiria ili kurahisisha mawasiliano,” alisema Mkuu wa wilaya.
Matukio katika ni muonekano wa juu kwa baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya Mlimba.

Awali Bi.Zainabu Makenjula Mkazi wa Mlimba ameomba serikali kushughulikia swala la barabara kwa wakati ili kurahisisha mawasiliano na kuwezesha wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji kwa sababu kuna maeneo magari wala pikipiki haviwezi kupita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news