Zanzibar na Saudi Arabia kuimarisha ushirikiano zaidi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameihakikishia Serikali ya Saudi Arabia ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Aprili 27,2024 Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Yahya Ahmad Okeish na ujumbe wake kwa lengo la kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya nchi mbili hizo.

Dkt. Mwinyi amesema, SMZ ni mnufaika mkubwa wa mfuko wa Saudia na Quwait kwenye miradi yake ya maendeleo kupitia ushirikiano mzuri uliopo baina ya mataifa hayo.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Saudi Arabia kwa ushirikiano wake na Tanzania hususani kuipatia Zanzibar zawadi mbalimbali inazozituma kwa watu wa Zanzibar ikiwemo tende wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Katika salamu zake kwa Tanzania, Balozi Okeish amepongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na taifa hili kwa kutimiza miaka 60 ya Muungano wake baina ya Tanganyika na Zanzibar sambamba na kuuombea mafanikio zaidi muungano huo.

Pia, Balozi Okeish alisifu ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Saudi Arabia na Tanzania ikiwemo Zanzibar pamoja na kusifu tamaduni za pande mbili hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news