Azam FC yawachezesha kwata mabao 2-0 maafande wa JKT Tanzania

DAR-Katika kipindi cha dakika 45 za kwanza, Abdul Hamisi Suleiman (Sopu) alizitumia vema naada ya dakika ya 30 kulipa bili ya waajiri wake.

Ni kupitia bao ambalo liliwafanya Azam FC kuongoza kipindi cha kwanza chote huku wenyeji wake, JKT Tanzania wakiambulia patupu.

Mtanange huo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara umepigwa Mei 21, 2024 katika dimba la Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo lililopo Mbweni jijini Dar es Salaam.

Aidha, kipindi cha pili, wawili hao waliendelea kuoneshana kandanda safi ingawa,Feisal Salim Abdallah (Fei Toto) dakika ya 90' naye aliziona nyavu za JKT Tanzania.

Matokeo hayo ya mabao 2-0 yanaifanya Azam FC kufikisha alama 63 ingawa inabaki nafasi ya pili nyuma ya Young Africans Sports Club ambao wana alama 71

Huku maafande wa JKT Tanzania kwa upande wao wakiwa na alama 31 za mechi 28 na wanashuka kwa nafasi moja hadi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news