Simba SC yaipiga Geita Gold FC mabao 4-1

DAR-Simba SC ya jijini Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Geita Gold kutoka mkoani Geita.
Ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao umepigwa Mei 21, 2024 katika Dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,Dar es Salaam.

Geita Gold walipata bao la kwanza kupitia kwa Jofrey Julius dakika ya 11 baada ya mlinda mlango Hussein Abel kukosea kucheza mpira wa krosi uliopigwa na Edmund John.

Baada ya bao hilo, Simba SC waliendelea kulishambulia lango la Geita Gold na kutengeneza nafasi, lakini walikosa umakini katika eneo la mwisho.

Saido Ntibazonkiza alisawazishia bao hilo dakika ya pili ya nyongeza kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Aidha,Geita Gold walimaliza mechi wakiwa pungufu kufuatia nahodha Michael Onditi kuoneshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 68 baada ya kumfanyia madhambi Willy Onana.

Ntibazonkiza alitupatia bao la pili dakika ya 71 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya Onana kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Vile vile, Ladaki Chasambi alitupatia bao la tatu dakika ya 85 baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Willy Onana.

Chasambi alipigilia msumari wa nne dakika ya 93 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.

Simba SC kwa ushindi huo inafikisha alama 63 ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 28.

Kwa upande wa Geita Gold inabaki na alama zake 25 za mechi 28 nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 ambayo imeonekana kuwa na ushindani mkubwa zaidi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news