Mama Mariam Mwinyi aishukuru Korea

ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi ameishukuru wadau wa maendeleo wa Korea kupitia Jumuiya ya Lady Fatima Charity kwa msaada wa dola za kimarekani 37,000 kwa ajili kuwezesha upatikanaji wa kutoa Taulo za kike (Tumaini Kits) zinazotengenezwa na ZMBF na zimenufaisha zaidi ya Wasichana 2,500 wa shule za Pemba.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo Mei 11,2024 alipokutana na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya kudumu ya Bunge la Korea , Mhe.Sul Hoon na ujumbe wake waliofika ofisini kwake Ikulu Migombani.
Mama Mariam Mwinyi amesema, ndoto yake ni kuwasaidia kuwainua kiuchumi Wanawake hususani wakulima wa Mwani kwa kuanzisha kiwanda kidogo cha kuchakata zao hilo , na amewakaribisha Serikali ya Korea katika kuendeleza ushirikiano na kujifunza zaidi kutoka kwao.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Kudumu ya Bunge la Korea, Mhe.Sul Hoon na ujumbe wake wameahidi kushirikiana na Taasisi ya ZMBF katika nyanja mbalimbali hususani vipaumbele vya taasisi hiyo.
Wabunge wengine walioshiriki ni pamoja na Mhe. Lee Hunseng na Mhe.Shin Hyun Young kutoka Bunge la Korea wanaojishughulisha na masuala ya mashirikiano na Bara la Afrika pia Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe.Kin Sun Pyo ameambatana na ugeni huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news