Young Africans Sports Club yaichakaza Dodoma Jiji FC kwa mabao 4-0

DODOMA-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwatembezea kichapo cha mabao 4-0 wenyeji Dodoma Jiji FC.
Kupitia, mtanange huo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao umepigwa Mei 22,2024 katika dimba la Jamhuri jijini Dodoma umewafanya walima zabibu kuwa wanyonge.

Clement Mzize alilipa bili kwa mwajiri wake dakika ya 10 ya mtanange huo kipindi cha kwanza huku, Stephanie Aziz Ki dakika ya 45' akifunga hesabu kipindi cha kwanza.

Katika dakika ya 51, Aziz Ki alirejesha tena maumivu kwa Dodoma Jiji FC huku Maxi Mpia Nzengeli akifunga hesabu la mabao manne dakika 78 ya mtanange huo.

Mabao hayo yanaifanya Young Africans Sports Club kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa kufikisha alama 74 za michezo 28.

Pia, hawa ndiyo mabingwa tena wa ligi hiyo, huku katika msimamo watani zao Simba SC wakiwa nafasi ya tatu kwa alama 63 baada ya mechi 28.

Aidha, nafasi ya pili inashikiliwa na Azam FC kwa alama 63 baada ya michezo 28, tofauti yake na Simba SC ni mabao tu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news