LATRA yatangaza nauli Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) Dar hadi Morogoro na Dar hadi Dodoma, tazama hapa

DODOMA-Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusu nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora baada ya kufanyia kazi maombi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Sambamba na maoni ya wadau wengine ambapo Dar es Salaam hadi Morogoro umbali wa kilomita 192nauli ni shilingi 13000 na Dar es Salaam hadi Dodoma kilomita 444 nauli ni shilingi 31,000.

Kwa mujibu wa LATRA, nauli hizi ni kwa daraja la kawaida kwa watu wazima na watoto kuanzia umri wa miaka 4 hadi 12 ambapo nauli zitalipwa na abiria kwa kilomita.

Aidha, nauli itakayolipwa na mtu mzima na mtoto mwenye umri zaidi ya miaka 12 ni shilingi 69.51 kwa kilomita na mtoto kuanzia kuanzia miaka 4 hadi 12 atalipia shilingi 34.76 kwa kilomita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news