Mbunge Dkt.Shogo Richard Mlozi afariki

DODOMA-Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya kusaidia wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi ya FUNGUA TRUST, Dkt.Shogo Richard Mlozi amefariki dunia.
Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson leo Juni 13, 2024 kabla ya kuanza kwa kikao cha 47 cha Mkutano wa Bunge la Bajeti.

“Leo asubuhi tumepokea taarifa kwamba Mheshimiwa Dkt. Shogo Richard Mlozi ambaye tulimchagua kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki hatunaye tena, hii ni taarifa ya awali tutakapopata taarifa za ziada tutawataarifu tusimame kaa dakika moja tumpe heshima zake za mwisho.”

Dkt.Mlozi ambaye alichaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika bunge hilo mwaka 2022 alikuwa anahudumu katika nafasi hiyo hadi 2027.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news