Orodha ya vijana wanaoitwa kwenye usaili kwa ajili ya kujiunga na Programu ya BBT-Life kupitia kundi la washiriki kutoka ndani ya Mkoa wa Pwani

NA GODFREY NNKO

OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kupitia Programu ya BBT-Life (Jenga Kesho Iliyo Bora) imesema,usaili kwa wale ambao wamekidhi vigezo ili kujiunga na programu hiyo utafanyika Juni 25 na Juni 26,2024 katika ofisi hiyo kuanzia saa 2:30 asubuhi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 18,2024 na Katibu Tawala wa mkoa huo,Rashid Mchatta.

"Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kupitia Programu ya BBT-Life imepitia maombi yote na kukagua nyaraka na sifa zilizoainishwa kwenye tangazo la maombi.

"Hivyo,inapenda kuwataarifu waombaji wote kuwa, usaili utafanyika Juni 25,2024 na Juni 26,2024 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuanzia saa 2:30 asubuhi."

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia mambo saba.

Mosi,kuzingatia tarehe walizopangiwa kufanyiwa usaili, pili wasailiwa waliowasilisha maombi yao kwa njia ya tovuti wanatakiwa kufika na fomu na viambatanisho vyote walivyotumia wakati wa maombi.

Tatu,wasailiwa wenye taaluma za mifugo na taaluma za taaluma nyingine wanatakiwa kufika na nakala zao za vyeti.

Nne,kila msailiwa atajigharamia kwa chakula,malazi na usafiri. Tano,waombaji waliomba kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) usaili wao utafanywa na JKT kwa utaratibu waliowekewa.

Sita,wasailiwa watakaopata nafasi ya kujiunga na BBT-Life watapewa taarifa zao kupitia tovuti ya Mkoa wa Pwani.

Saba, kwa mujibu wa taarifa hiyo, waombaji wengine ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili, watambue kuwa hawakukidhi vigezo.

"Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi nyingine za kushiriki zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika,"amesisitiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani,Rashid Mchatta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news