Gavana Tutuba ajumuika na magavana 60 mkutano muhimu Uswisi

BASEL-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba pamoja na magavana 60 wa Benki Kuu kutoka mataifa mbalimbali duniani wamehudhuria Mkutano wa Mwaka wa 94 wa Taasisi ya Kimataifa ya fedha ya Benki Kuu uliofanyika Basel, Uswisi kuanzia tarehe 28 hadi 30 Juni 2024.
Gavana Tutuba pia alihudhuria mkutano wa Magavana wa Benki Kuu za Afrika ulioratibiwa na Kituo cha Utafiti wa Uchumi wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Oxford kuanzia tarehe 1 hadi 3 Julai 2024.
Mikutano hii hufanyika kila mwaka ambapo Magavana wa Benki Kuu hupata fursa ya kujadili masuala ya kifedha ya kimataifa na kikanda, kubadilishana uzoefu, na kushirikiana katika kutafuta suluhisho za changamoto mbalimbali za kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news