Katibu Mkuu Msigwa anadi fursa za uwekezaji Sanaa na Michezo kwa Urusi

DAR-Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ametoa wito kwa wawekezaji kutoka nchini Urusi waje kuwekeza nchini Tanzania kwenye Sekta ya Sanaa na Michezo kwa kuwa Tanzania imeshaweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta hizo na Sekta nyingine.
Katibu Mkuu Msigwa ametoa wito huo Julai 10, 2024 jijini Dar es Salaam, katika Siku ya Urusi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade) kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba) yanayoendelea jijini humo.
Amesema, Tanzania na Urusi zina ushirikiano katika Sekta ya Biashara ambapo bidhaa za Tanzania zenye thamani ya dola za Marekani milioni 6.4 zinauzwa Urusi na bidhaa za Urusi za thamani ya Dola za Marekani milioni 179 nchini Tanzania hivyo Watanzania wanayo nafasi ya kujifunza zaidi kutoka katika nchi hiyo.
Amewataka watanzania watumie majukwaa kama hayo ya kukutana na wafanyabiashara wa Kimataifa kujifunza zaidi katika eneo la ujuzi, kukuza mitaji pamoja na teknolojia ili kuongeza thamani ya biashara zao kimataifa.
Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Andrey Avetsyan amesema,nchi hiyo inafurahishwa na ushirikiano uliopo miongoni mwa nchi hizo, akieleza kuwa nchi hiyo ipo tayari kuongeza ushirikiano katika maneno mengi zaidi hasa teknolojia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news