Magazeti leo Julai 11,2024

MOROGORO-Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka amesema, dereva na msaidizi wake wa lori la mizigo lililoteketea kwa moto baada ya kupata ajali likiwa linaelekea Burundi usiku wa kuamkia Julai 10,2024 eneo la Kwambe-Dumila wilayani humo wamefariki.
Mheshimiwa Shaka amesema,katika ajali hiyo watu watatu wamefariki wote wanaume ambao ni dereva wa lori na msaidizi wake raia wa Burundi pamoja na dereva wa gari dogo ambaye amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya St. Joseph Dumila.
Lori hilo liligongana na gari dogo aina ya Harrier lenye namba za usajili T.593 DVA katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma na kisha lori likatumbukia kwenye korongo ambapo juzi usiku DC Shaka alifika eneo la tukio.
Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news