Wasanii wa Tanzania wakutana na mastaa wa Korea, wayajenga pamoja

SEOUL-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Korea, Togolani Edriss Mavura ameambatana na wasanii aliowaalika kufanya ziara nchini Korea Kusini na kukutana na msanii mkubwa nchini humo Ye-Jin kwa lengo kuimarisha mahusiano na kubadilishana ujuzi katika soko la filamu na kubadilishana mawazo ya namna ya kuendeleza sekta hiyo kimataifa.

Aidha,wamekutana na watengeneza filamu wakubwa Cheol-ha Lee na Yohwan KIM.
Director Cheol-ha Lee amesema,yupo katika maandalizi ya filamu itakayohusisha waigizaji wa Kimataifa na angependa kupata muigizaji kutoka Tanzania kwa Afrika.

Katika kikao hicho, wasanii hao wametoa mawazo mbalimbali ikiwemo Serikali kuweka nguvu katika kuinua wasanii wadogo ili kukuza na kuendeleza vipaji.
Aidha wamepokea mwaliko kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, kuja Tanzania kuchagua maeneo mbalimbali ya kufanyia filamu zao na kisha kutembelea vivutio maridhawa vinavyopatikana Tanzania.
Wameshukuru kwa zawadi za shuka za kimasai walizovalishwa na kiongozi wa msafara Steve Nyerere, msanii Irene Uwoya na Blandina Chagula (Johari).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news