Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa ZRA aagwa

ZANZIBAR-Leo ilikuwa ni hafla ya kumuaga aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ambaye kwa sasa ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) CPA. Yusuph Juma Mwenda.Matukio mbalimbali katika picha wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ambaye kwa sasa ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),CPA Yusuph Juma Mwenda.
Hafla hiyo imefanyika leo Jumamosi Julai 6, 2024 Makao Makuu ya ZRA Mazizini- Unguja.Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum.

Wafanyakazi mbalimbali wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), viongozi mbalimbali wa Serikali wamehudhuria hafla hiyo ya kuagwa kwa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ambaye kwa sasa ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Ikumbukwe kua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan alimteua,  CPA Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) siku ya Jumanne Julai 2,2024 na baadae kuapishwa Julai 5,2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news