PWANI-Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu,Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewashukuru wananchi kwa kuendelea kuonesha imani kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ni baada ya kukipa chama hicho ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika Novemba 27,2024 nchini.
Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amesema, katika uchaguzi huo CCM Chalinze ilishinda vijiji vyote 74, vitongoji vyote 469 na wajumbe wote.
"Nimepata nafasi ya kutoa nasaha katika mkutano na wenyeviti wa vijiji,vitongoji na wajumbe wa halmashauri za vijiji katika makundi yote wapatao 1919 uliofanyika Lugoba, Chalinze mapema leo Novemba 30,2024.
"Nimetumia nafasi hiyo kuwakumbusha wajibu wao kwa wananchi, Serikali zao na kwa chama chao. Pia nimewatakia kheri katika majukumu yao kwa jumla na kuwaahidi ushirikiano mkubwa sana toka kwangu na ofisi yangu."
Ameyabainisha hayo leo Novemba 30,2024 katika mkutano na na wenyeviti wa vijiji,vitongoji na wajumbe wa halmashauri za vijiji katika makundi yote wapatao 1,919 uliofanyika Lugoba, Chalinze mkoani Pwani.