DAR-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Bo Li, mazungumzo yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam leo Januari 28,2025.

Amesema kupitia programu hizo, zimechangia ukuaji wa uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei na ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi.

Aidha ameipongeza Tanzania kwa kutekeleza vyema programu ya ECF na kupata alama za juu katika tathimini ya nne.