RIYADH-Serikali imekemea watanzania wanao kwenda kufanya kazi nje ya nchi bila kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa inasababisha kutojulikana walipo na shughuli wanazozifanya.

Aidha, amesema uhusiano mazuri uliopo baina ya Tanzania na nchi ya Saudi Arabia hawataruhusu wafanyakazi kufanya kazi au kusafiri bila kufuata utaratibu, hivyo kila mtanzania anayehitaji kufanya kazi nje ya nchi apitie kwa mawakala wanatambulika baina ya nchi hizo mbili.
Mhe. Ridhiwani amesema miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa watanzania kusafiri kwenda nchini Saudi Arabia, upimaji wa Afya zao, kupata kazi zenye staha na mshahara mzuri ambao utawasaidia kujikwamua kiuchumi.