DODOMA-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kimeandaa mpango wa kuanza kutoa mafunzo ya uandishi wa habari za michezo chuoni hapo.
Waziri Prof. Kabudi ameyasema hayo leo wakati Akichangia mjadala wa taarifa ya kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2024 leo Februari 11, 2025 ambapo ameeleza kuwa chuo hicho kimeandaa mpango huo ili kuwawezesha wachambuzi kuwa na weredi katika kuandaa habari za michezo.Aidha, Waziri Kabudi amesema kuwa Serikali imetenga Shilingi Bilioni moja na Milioni Mia Tano (1,500,000,000) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho kilichopo Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.