LINDI- Basi lililobeba wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Dodoma Jiji limepinduka na kutumbukia mtoni katika eneo la Nangurukuru mkoani Lindi likiwa na wachezaji.
Ajali hiyo imetokea Februari 10, 2025 ambapo kikosi hicho kilikuwa kikitokea Ruangwa mkoani Lindi kurejea mkoani Dodoma, baada ya mchezo wao wa Februari 9,2025 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania dhidi ya Namungo FC.Katibu Mkuu wa timu hiyo, Fortunatus Johnson amethibitisha tukio hilo akieleza kuwa wachezaji wote wamejeruhiwa kwa kukatwa na vioo vya gari.
Dodoma Jiji FC kupitia mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa dhidi ya wenyeji Namungo FC waliambulia sare ya mabao 2-2.