DAR-Wafanyabiashara 774 kati ya 1,520 waliotambuliwa kuwa na sifa za kurejeshwa katika soko la Kariakoo wamejitokeza leo katika ukumbi wa mikutano wa Arnautoglo Dar es Salaam kuchukua fomu maalum za usajili kwa ajili ya maandalizi ya kuingia kwenye soko hilo kufuatia tangazo la kukamilika kwa uhakiki wa wafanyabiashara na majina kutangazwa kwa umma
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo leo imeonesha kuwa kazi ya kuchukua, kujaza na kisha kurejesha fomu hizo imeanza leo na itakamilika siku ya Ijumaa tarehe 7 Februari 2025 kisha taratibu za uchukuaji na ujazaji wa mikataba kati ya Shirika na mfanyabiashara itaendelea.
