Waziri Kombo afanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi nchini

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud T. Kombo (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uswisi nchini, Mhe. Nicole Providoli yaliyofanyika katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam tarehe 18 Februari 2025.
Madhumuni ya mazungumzo hayo yalikuwa ni Mhe. Providoli kujitambulisha rasmi kwa Mhe. Waziri Kombo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Novemba 2024.

Aidha katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekata ya Afya, maji, TEHAMA, madini na ufadhili wa masomo.
Wamekubaliana pia kuimarisha ushirikiano katika eneo la biashara na uwekezaji kupitia Switzerland-Tanzania Chamber of Commerce (STCC) iliyozinduliwa nchini mwezi Februari 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news