KILIMANJARO-Wanakwaya sita wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), usharika wa Chome wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wamefariki dunia huku wengine 23 wakijeruhiwa, baada gari lao kupata ajali.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Same, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Kasilda Mgeni, amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi.Amesema, wanakwaya hao walikuwa wakitokea Chome kuelekea Vudee kueneza Injili kwa njia za nyimbo na walipofika barabara ya Bangalala wakapata ajali.
Chanzo cha ajali hiyo ni gari aina ya Costa walilokuwa wakisafiria, kushindwa kupanda mlima kisha kuangukia bondeni.
Majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same, wakiendelea kupatiwa matibabu na miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini hapo.