DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia Tawi lake la Dodoma imeendesha mafunzo ya siku moja kwa kundi la watu wenye mahitaji maalumu kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu majukumu yake, namna ya kutambua alama za usalama kwenye fedha, pamoja na mbinu bora za kuzitunza.
Katika mafunzo hayo, washiriki walielezwa umuhimu wa Benki Kuu kama muhimili wa uchumi wa nchi, ikizingatiwa kuwa jukumu lake kuu ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.

