VIDEO:Viongozi wenzangu CHADEMA walitaka kuniua-Siglada Mligo

NJOMBE-Mwenezi wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAVICHA), Siglada Mligo, ameendelea kufichua kwa undani tukio lililompelekea kupigwa na hatimaye kulazwa hospitalini akiwa katika hali mahututi.
Kwa mujibu wa Mligo, tukio hilo lilitokea wakati wa kikao cha ndani cha wanachama wa CHADEMA kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche. Kikao hicho kilifanyika mara baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika siku hiyo.

Mligo anadai kuwa wakati wa kikao hicho, alimuomba Heche fursa ya kuzungumza ili kuweka wazi baadhi ya masuala kwa ajili ya mustakabali wa chama.

Hata hivyo, badala ya kupokelewa kwa hoja zake, alijikuta akikaripiwa vikali na Heche, hatua iliyofikia hadi kutolewa nje ya kikao kwa nguvu.

Baada ya kufukuzwa kutoka kikaoni, Mligo anasema alimtumia Heche ujumbe wa simu akiomba kuruhusiwa kurejea na kutoa mchango wake.

Hata hivyo, badala ya kujibiwa, alidai kuwa kundi la vijana lilitumwa kumfuata, miongoni mwao akiwa mlinzi wa Heche, ambaye alimshambulia vibaya na kumsababishia majeraha makubwa.

Kwa mujibu wa Mligo, kilio chake cha maumivu kilisababisha askari waliokuwa kwenye doria kuingilia kati na kumsaidia. Askari hao walimkimbiza katika kituo cha afya kwa ajili ya matibabu.

Ukiangalia mlolongo wa tukio hili, ni dhahiri kuwa shambulio dhidi ya Mligo lilifanywa kwa makusudi, kwa lengo la kumzuia kushiriki tena kwenye kikao hicho.

Swali linabaki: Je, CHADEMA kweli ni chama cha demokrasia? Chama kinachojiita cha kidemokrasia kinaweza kumdhuru mwanachama wake, tena mwanamke, kwa sababu ya tofauti za kimtazamo?

Ni wazi sasa kwamba CHADEMA chini ya uongozi wa Tundu Lissu na John Heche kinaendeshwa kwa mkono wa chuma. Wale wote wanaoonekana kuwa wafuasi wa Freeman Mbowe au wasioonyesha utii kwa Lissu wanachukuliwa kama maadui.

Tunatoa wito kwa wanaharakati wa haki za binadamu na haki za wanawake kupaza sauti kwa niaba ya Siglada Mligo. Ni muhimu kuhakikisha anapata haki yake na pia kushinikiza CHADEMA na Heche kumuomba msamaha na kugharamia matibabu yake kikamilifu.

Ukatili huu haupaswi kufumbiwa macho. Ni muhimu kuukemea sasa kabla uongozi huu wa CHADEMA haujafikia hatua ya kuhatarisha maisha ya wanachama wao kwa sababu tu ya tofauti za kimtazamo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news