DAR-Meneja Habari na Mawasiliano wa Young Africans Sports Club (Yanga SC),Ally Kamwe amepewa adhabu ya kulipa faini ya shilingi milioni 5 na onyo la kutofanya kosa la kimaadili ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Ni baada ya kukutwa na hatia katika tuhuma ya kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni za Maadili ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Toleo la Mwaka 2021.
Adhabu hiyo ambayo imeanza kufanya kazi Aprili 16, 2025 imetolewa na Kamati ya Maadili ya TFF katika kikao chake cha kupitia na kutolea uamuzi mashauri yaliyowasilishwa mbele yake.
Kwa upande mwingine Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Sports Club,Ahmed Ally ameachiwa huru.
Ni baada ya kamati kubaini kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumuingiza hatiani kwa kosa aliloshtakiwa na Sekretarieti ya TFF akituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni za Maadili ya TFF.