DAR-Wakati vitisho vya kimtandao vinaendelea kutajwa kuongezeka duniani, Tanzania inaendelea na juhudi za kulinda miundombinu yake ya kidijitali, kwa kuandaa kwa mara nyingine jukwaa kubwa la Usalama Mtandaoni.
Jukwaa hilo linalotarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Aprili 10,mwaka huu katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha, linadhihirisha dhamira ya dhati ya nchi ya kuimarisha uimara wa mifumo ya kimtandao.
Aidha,jukwaa hilo litakutanisha viongozi wa sekta, watunga sera, wataalamu wa TEHAMA, wabobezi wa usalama mtandaoni wa ndani na nje ya nchi na wadau mbalimbali.

"Mabadiliko ya haraka ya kidijitali nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla yameleta fursa nyingi, lakini pia yamefungua mianya ya hatari za kisasa za kimtandao.
“Mkutano huu ni jukwaa muhimu la kushirikiana maarifa, kuimarisha uwezo, na kujenga ushirikiano ili kuhakikisha usalama wa mazingira ya kimtandao ndani na nje ya nchi yetu."
Alisema, jukwaa hilo limeandaliwa kwa kushirikiana na wadau muhimu kutoka taasisi za serikali, sekta binafsi, na mashirika ya kimataifa ya usalama mtandaoni.
Pia, amesema kupitia jukwaa hilo, wanalenga kuimarisha uimara wa mifumo dhidi ya hatari mbalimbali za kimtandao, kuongeza uelewa, na kuhimiza matumizi ya mbinu bora za usalama katika mazingira ya kidijitali.
Pia litagusia mwelekeo wa sasa katika masuala ya usalama mtandaoni, ikiwa ni pamoja na matumizi ya Akili Unde (AI), Ulinzi wa Taarifa, na matishio mapya dhidi ya biashara na watu binafsi.
Kadri uhalifu wa kimtandao unavyozidi kuongezeka, ni muhimu kwa biashara, taasisi za serikali, na watu binafsi kuchukua hatua za mapema za kujilinda dhidi ya vitisho hivyo na kulinda taarifa nyeti pamoja na miundombinu yake muhimu.
Jukwaa hilo linaendana na Dira ya Tanzania ya kuwa na Uchumi wa Kidijitali ulio salama na wenye mafanikio.
Hata hivyo, jukwaa hilo litaongozwa na kaulimbiu isemayo, "Kuimarisha Uimara na Kukabiliana na Vitisho Katika Uchumi wa Kidijitali".
Mambo Muhimu katika Jukwaa:
■Mawasilisho yenye ubora ya Wataalamu - Maoni na uelewa kutoka kwa wataalamu wa usalama mtandaoni na wawakilishi wa Serikali.
■Majadiliano ya Wadau – Mijadala ya wazi kuhusu vitisho, sera na mikakati ya kukabiliana navyo.
■Warsha na Maonesho ya Moja kwa Moja – Mafunzo kwa vitendo na kuonesha suluhisho mpya za usalama.
■Fursa za Kuunganisha Wadau – Kukutana na viongozi wa sekta, wasimamizi, na wataalamu wa usalama mtandaoni.
Kuhusu Tume ya TEHAMA (ICTC)
Tume ya TEHAMA (ICTC) ni Taasisi ya Serikali yenye jukumu la msingi la Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya TEHAMA nchini.
Pia Tume ina majukumu ya kukuza na kuvutia uwekezaji wa TEHAMA, kuendeleza wataalamu wa TEHAMA pamoja na kuimarisha uratibu wa shughuli za TEHAMA ili kuongeza mchango wa TEHAMA katika Pato la Taifa.
Usajili
Je, ungependa kushiriki na kuwa sehemu ya mjadala huu muhimu? Kwa msaada wa kujisajili wasiliana na:
Esther Brown – 0764 643 546.
Innocent Shayo – 0719 995 944.
Thomas Joseph - +255 623 960 383.
Barua pepe: info@ictc.go.tz
Simu/WhatsApp (Ofisi): +255 736 848 444
Udhamini:
Kwa fursa za udhamini na ushirikiano, tafadhali wasiliana nasi kupitia: Simu (Mhandisi Jasson Ndanguzi): 0765 709 122.
Jiunge nasi katika kuunda mustakabali salama wa kidijitali kwa Tanzania!.