MAPUTO-Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad amewasili kituo chake cha kazi jijini Maputo.
CP Hamad ambaye aliteuliwa Desemba 8,2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Balozi alipangiwa kituo hicho Machi 25,2025.

Kabla ya uteuzi huo, Mheshimiwa CP Hamad alikuwa ni Kamishna wa Polisi Zanzibar. Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji pia anawakilisha mataifa ya Madagascar na Eswatini.