IRINGA-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaomba viongozi wa dini nchini kuliombea Taifa wakati huu wakati Tanzania inaelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani ili kuendelea kuwa na amani.


“Wito wangu kwa kanisa ni kuendelea kuliombea Taifa liendelee kuwa na amani,” amesema na kuongeza kuwa atamtamtaatifu Mhe. Rais kuhusu ahadi ya maaskofu kuliombea taifa hili kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amempongeza Askofu Mihali kwa wadhifa huo na kumshauri kutumikia watu akizingatia kuwa yeye ni mwanadamu aliyeinuliwa kati ya wanadamu na kuwekwa kati yao ili awatumikie.
Amemtaka kuongoza na kuwaelekeza huku akiwaonya kwa uvumilivu utakaotokana na kuomba baraka za Mungu.
"Kumbuka kuwahudumia mapadre, mashemasi, watu masikini na wageni wanaohitaji huruma yako nawe utakuwq umefanya kazi ya kitume,”amesema Kardinali Pengo.
Pia amemtaka kushirikiana na makanisa yote hasa yanayohitaji msaada ambapo amesema kufanya hivyo atakuwa ametimiza maelekezo ya Kanisa.
Aidha, amewataka waumini kumpokea kiongozi wao kwa moyo wa shukrani na furaha huku wakimheshimu kama mtumishi wa kristo.
Naye Makamu wa Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Eusebius Nzigilwa ameipongeza Serikali kwa ushirikiano wake na madhehebu ya dini nchini.
"Mgeni rasmi ambaye umemwakilisha mheshimiwa Rais, tunakushukuru kwa kuungana nasi na hii insonesha namna Serikali inavyothamini na kulinda uhuru wa kuabudu nchini,"amesema.
Aidha, Askofu Nzigilwa ameiomba Serikali kuendeleza ushirikiano na madhehebu ya Dini.
Pia Askofu Nzigilwa amewahimiza waumini wakatoliki kuliombea Taifa wakati huu kuelekea Uchaguzi Mkuu ili taifa liendelee kuwa na mani, umoja na mshikamano.
Amewataka watanzania kuchagua viongozi, wenye uwezo, wazalendo wanaoishi kwa kuzingatia misingi ya haki na uadilifu kwa maendeleo na Ustawi wa Taifa.
Mwakilishi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Angelo Ankantino amemshukuru Askofu mstaafu Ngalalekumtwa kwa maboresho, amenshukuru kwa huduma bora kwa kanisa.
Amentaka Askofu mpya kuwa kiongozi mwema mwenye moyo wa upendo na kujali, mwenye unyenyekevu huku akilinda haki kwa wote.

Akizungumza baada ya kusimikwa, Askofu Mihali amempongeza Dkt. Biteko kwa hotuba ambayo amesema imejawa ubunifu mbinu zenye mvuto kwa wasikilizaji.
Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hatua yake ya ukinara wa kuendelea kuwaunganisha Watanzania.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na maelfu ya wananchi wakiwemo maaskofu, mapadre, mafrateli, watawa wa kike na wakiume pamoja na viobgozi mbalimbali wa Serikali na wabunge.