Dkt.Kikwete awasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Dkt.Samia kwa Rais wa Guinea ya Ikweta

MALABO-Rais Mstaafu wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasilisha Ujumbe Maalum ambao ulipokewa na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Guinea ya Ikweta, Mhe. Simeon Oyono Esono Angue, kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo, Mhe. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.
Uwasilishaji wa ujumbe huo ulifanyika katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Malabo tarehe 13 Aprili 2025.
Katika tukio hilo, Mhe. Kikwete pia alitoa salamu za Rais Samia, akisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano, mshikamano, na umoja ili kukabiliana kwa pamoja na changamoto zinazokabili Bara la Afrika na dunia kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news