WASHINGTON-Mtanzania,Ahmed Fuad Edha ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azania Group ametunukiwa udaktari wa heshima wa ujasiriamali kutoka Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani.
“Tunampongeza kwa dhati Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Group of Companies kwa kutunukiwa Udaktari wa Heshima wa Ujasiriamali kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, taasisi maarufu duniani kwa ubora na ubunifu.
"Heshima hii ni ushuhuda wa uongozi wake wa kipekee, maono na mchango mkubwa katika kubadilisha maisha ya maelfu ya familia kupitia biashara na fursa Kusini mwa Bara la Afrika. Hongera sana kwa heshima hii muhimu,"imeeleza sehemu ya taarifa kutoka Chuo Kikuu cha Harvard.