Dkt.Natu ateta na Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji ya Dhamana

DAR-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji na Dhamana (Capital Market Tribunal), Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga, ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Mwanza, na kulishauri Baraza hilo kujitambulisha na kujitangaza kwa umma ili wadau waelewe uwepo wake kutokana na umuhimu wa Baraza hilo katika kusimamia mashauri ya masuala ya masoko na mitaji.
Baraza hilo lilianzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 136A cha Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Sura ya 79 (marekebisho ya sheria ya mwaka 2010), kama Baraza linalojitegemea ambapo kwa mujibu wa sheria, Baraza limepewa mamlaka kamili, sawa na Mahakama Kuu ya Tanzania katika kutekeleza majukumu yake.
Aidha, lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kuimarisha usimamizi wa haki katika sekta ya masoko ya mitaji kwa kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusiana na sekta hiyo kwa haki, weledi, na ufanisi.

Dkt. Natu El-maamry Mwamba alimhakikishia Mhe. Jaji kwamba Wizara ya Fedha, ambayo ndiyo msimamizi wa Baraza hilo itaendelea kutoa ushirikiano na kuliwezesha kutekeleza majukumu yake ili kuwakilisha kuwa linatimiza malengo ya kuanzishwa kwake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news