Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) yaibuka Mshindi wa Kwanza katika Maonesho ya Kwanza ya Mfuko wa Utamaduni nchini

DAR-Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma katika Maonesho ya Kwanza ya Mfuko wa Utamaduni yaliyofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Aprili, 2025 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
TEA ilikuwa miongoni mwa taasisi zaidi ya 30 zilizoshiriki katika maonesho hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Utamaduni, kwa lengo la kuhamasisha na kuendeleza shughuli za kitamaduni nchini.
Vigezo vilivyotumika katika kutoa tuzo hizo ni pamoja na muonekano wa banda, utoaji wa huduma kwa wageni waliotembelea banda, pamoja na muda wa kufungua na kufunga huduma.

Tuzo hizo zilitolewa na Mgeni Rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Prof. Paramaganda Kabudi, ambaye alipongeza taasisi zote zilizoshiriki kwa mchango wao katika kufanikisha maonyesho hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news