Rais Dkt.Samia ateua viongozi mbalimbali

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:-

Arch Dkt. Fatma Kassim Mohamed ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa kipindi cha pili;

Balozi Dkt. Jilly Elibariki Maleko ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Balozi Maleko anachukua nafasi ya Balozi Begum Karim Taj ambaye amemaliza muda wake;

Prof. Eliakimu Mnkondo Zahabu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (National Carbon Monitoring Center – NCMC); na

Bw. Lucas Abrahamani Mwino ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA). Bw. Mwino anachukua nafasi ya Dkt. John Kedi Mduma ambaye amemaliza muda wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news