ZANZIBAR-Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) limehamishia mashindano ya Muungano 2025 na kuyapeleka kenye uwanja wa Gombani Pemba, kwani mashindano hayo awali yalipangwa kufanyika Unguja katika dimba la New Amaan Complex.
Taarifa ya Kaimu Afisa Habari wa ZFF, Issa Chiwile imesema imeamua kuyapeleka mashindano hayo kwenye Uwanja wa Gombani baada ya kupata maelekezo ya kitaalamu kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuhusu namna ya kuutunza uwanja huo wa New Amaan Complex.
Kwa sasa dimba la New Amaan Complex limeingia kwenye mfumo maalumu wa matumizi ya CAF, pia sehemu yake ya kuchezea (Pitch) inahitaji muda zaidi wa kuimarika, hivyo haihitajiki kuchezwa michezo mingi kwa sasa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) imeyahamishia mashindano ya Kombe la Muungano kutoka Uwanja wa New Amaan Complex kwenda Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba. Ni kutokana na maelekezo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) kutaka uwanja wa New Amaan Complex kutotumika kwa michezo mingi mfululizo.