ZANZIBAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa kuridhia Mashindano ya AFCON na CHAN kufanyika nchini utasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza na kukuza sekta ya michezo na utalii nchini.

“Ujio wa wageni wakati wa michuano utahitaji malazi, chakula na usafiri hivyo waliowekeza kwenye hoteli na vyombo vya usafiri watapata faida kubwa na kujiingizia kipato, hii ni fursa nzuri ambayo Marais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi wametuletea kwa sababu timu zinakuja na watu wengi.”
Aidha,Mheshimiwa Majaliwa amesema ameridhishwa na kasi na bora wa ukarabati wa viwanja hivyo unaofanywa na kampuni za REFORM na ORKUN “Kampuni hizi zimetujengea viwanja vilivyo na ubora unaokubalika”.
Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa jukumu lililopo kwa sasa ni kuilinda miundombinu hiyo ili ubora uliofikiwa baada ya ukarabati uendelee kuwepo hadi michuano hiyo itakapofanyika.
“Watanzania wanatamani kuvitumia viwanja hivi lakini wanatakiwa wajue kwamba viwanja hivyo kwa sasa viko kwenye ukaguzi maalum unaofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika hivyo ni muhimu kuweka utarabu ambao hautaathiri ubora ulipo”.

Pia, Waziri Mkuu amesema mashindano hayo yataleta manufaa makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii na biashara. "Hii ni fursa nzuri ambayo Marais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi wametuletea kwa sababu timu zinakuja na watu wengi."
