Mradi wa Urekebu ulibaini marekebisho yanahitajika kufanyika kwa njia ya sheria ya Bunge-Mwanasheria Mkuu wa Serikali

DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Hamza Johari amesema, wakati wanafanya Mradi wa Urekebu walibaini baadhi ya marekebisho yanahitajika kufanyika kwa njia ya sheria ya Bunge.
Hivyo wizara iliandaa muswada kwa ajili ya kutungwa kwa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali yaliyotokana na zoezi la Urekebu.

Pia, ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa mchango kwa kipekee ambao ulifanikisha mradi huo.

Mheshimiwa Johari ameyasema hayo leo Aprili 23,2025 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa Toleo la Sheria zilizofanyiwa Urekebu kwa mwaka 2023.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Wakati tunatekeleza mradi huu wa Urekebu tulibaini kuwa,baadhi ya maboresho yanahitaji kufanyika kwa njia ya Sheria ya Bunge, hivyo wizara iliandaa muswada kwa ajili ya kutungwa kwa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali yaliyotokana na zoezi la Urekebu.

"Sheria Na.3 ya mwaka 2023, ninaishukuru sana wizara kwa kufanikisha hili, hivyo tukaweza kuendelea na zoezi la utekelezaji wa mradi."

Ameeleza kuwa, Urekebu wa Sheria ni mradi walioufanya kwa ajili ya kufanya majumuisho ya marekebisho ya sheria mbalimbali yanayofanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lengo la kufanya hivyo, amesema ni ili kuwa kitu kimoja kurahisisha upatikanaji,usomaji na utumiaji wa sheria hizo.

"Ni kazi ya msingi inayolenga kuhuisha, kuboresha na kurahisisha matumizi ya sheria za nchi yetu."

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa, kwa kufanya hivyo wanahakikisha sheria za nchi zinakuwa hai,zinaenda na wakati na kueleweka kwa urahisi na wananchi wote.Amesema,zoezi hilo limehusisha wananchi wote nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news