DAR-Mwandishi wa habari wa siku nyingi, Rahabu Fred Fungo aliyekuwa mhariri katika kituo cha habari cha Azam Media, amefariki dunia leo April 5, 2025 akiwa anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Rahabu aliyekuwa mke wa aliyekuwa mtangazaji mahiri, marehemu Fred Fidelis maarufu Fredwaa, alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
"Uongozi wa kampuni ya Azam Media Limited, unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi wake, Rahab Fred Fungo, aliyekuwa Mhariri Mkuu Msaidizi kwenye Idara ya Habari na Matukio.
"Rahab amefariki dunia Aprili 5, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
"Azam Media Limited inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza kifo cha mpendwa wetu."
