Rais Dkt.Mwinyi kuelekea Uingereza kushiriki Mkutano wa CTIS

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ataondoka nchini leo kuelekea jijini London, nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 6 hadi 9 Aprili 2025 kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Trade & Investment Summit 2025).
Katika ziara hiyo, Rais Dkt.Mwinyi matukio mengine atakayoshiriki ni kukutana na Viongozi waandamizi wa Serikali ya Uingereza na Taasisi zake, atakutana na Diaspora wa Tanzania waliopo nchini Uingereza, atakutana na Sir Tony Blair, Waziri Mkuu Mstaafu na Kiongozi wa Tony Blair Institute (TBI), pia atakutana na wadau wa uwekezaji katika uchumi wa bluu.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi atakutana na wadau wa uwekezaji katika sekta ya utalii, filamu, viwanda, nishati ikiwemo pia mafuta na gesi.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi atashuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano baina ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Chuo Kikuu cha Kent kwa ajili ya utafiti wa kilimo cha Mwani pamoja na MOU kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Perry Engineering ya Uingereza kuhusu usambazaji wa mbegu za mwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news