NLD yapitisha wagombea Urais Uchaguzi Mkuu 2025

DAR-Chama cha National League for Democracy (NLD) kimemuidhinisha,Doyo Hassan Doyo kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 huku Mfaume Khamisi Hassani akiidhinishwa kuwania Urais wa Zanzibar.
Akizungumza baada ya uchaguzi,Doyo amesema chama hicho kinapenda Taifa la Tanzania na hawapo tayari kujihusisha na chama chochote kutoshiriki uchaguzi, hivyo watashiriki zoezi hilo mpaka mwisho na watalinda tunu ya amani iliyopo.

Kwa upande wake,mgombea Urais Zanzibar,Mfaume Khamisi Hassani ameshukuru kwa chama hiko kumuamini kwenda kupeperusha bendera ya NLD na atahakikisha Wazanzibari wakimpatia kura,Serikali itakayoundwa itashughulika na utatuzi wa kero zote za wananchi.

Aidha, kwa sasa baadhi ya vyama kati ya vyama 19 vyenye usajili wa kudumu vimetangaza na kupitisha wagombea urais wao.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano maalum mwezi Januari, 2025 walimpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kutetea nafasi ya urais na Makamu wake ni Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.

Pia, Rais Hussein Ali Mwinyi alipitishwa kuendelea kutetea nafasi hiyo kwa upande wa Zanzibar.

Vile vile,Chama cha NCCR Mageuzi kimewateua Ambar Khamis kupeperusha bendera ya urais huku mgombea mwenza akiwa ni Joseph Selasini.

Wateule hao ambao ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa, na Makamu Mwenyekiti,wamepitishwa Machi 29, mwaka huu katika mkutano mkuu uliofanyika jijini Dodoma na kuwaleta pamoja wanachama wa chama hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news