Na Guillaume Vld
SI watu wengi wanafahamu kwamba Vatikani ina maktaba ya chini ya ardhi, yenye urefu wa zaidi ya maili 50 (sawa na zaidi ya kilomita 80).
Katika maktaba hiyo ya ardhini, pia kuna shehena ya hifadhi ya vitu ambavyo vina siri ya historia ya ulimwengu.
Ndio, narudia kusema, maktaba ya ardhini yenye urefu wa maili 50, ambapo hii sio dhana wala habari ya nadharia; ni ukweli usiopingika.
Kumbukumbu za Siri ya Vaticani (Vatican Secret Archives), ni halisi na ziko katika mojawapo ya tovuti za Vaticani ambazo ni mahsusi kwa ajili ya masuala ya kidini na kitamaduni duniani.
Aidha, kumbukumbu hizo za jumla ya urefu wa maili 53 zimepangwa vizuri katika mashelvu yenye katalogi 35,000, zikiwemo dokumenti ambazo zina umri wa zaidi ya miaka 1,200.
Jina "Kumbukumbu za Siri" linaongeza usiri katika hizo siri zao nyingi, ambazo hujumuisha mambo ya siri za hii dunia zilizofichwa katika kile kinachoitwa Stori za Kiza (dark stories).
Kwa kuwa hizo faharasa (indexes) si za wazi kwa umma na zinaweza kupatikana tu kwa wanasayansi wa taaluma flani pekee, watu wengi wanafikiri kwamba kumbukumbu hizo zina mambo ya kushtua au hata ya ajabu.
Baadhi ya watu wanaofahamu uwepo wa siri hizo na ambao hawana uwezo wa kwenda huko ardhini kuzipekua, wanaamini kwamba huenda Vatikani inaficha ukweli kuhusu viumbe wa kigeni (aliens) kutoka anga au sayari zingine.
