Waziri Kombo asaini Kitabu cha Maombelezo Ubalozi wa Vatican nchini

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amesaini kitabu cha maombelezo katika Ofisi za Ubalozi wa Vatican nchini zilizopo Oysterbay jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis.
Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, kwa miaka 12 alifariki dunia tarehe 21 Aprili, 2025 nyumbani kwake katika mji wa Vatican kutokana ugonjwa wa Kiharusi.
Waziri Kombo ametia saini kitabu hicho cha maombelezo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza ubalozini hapo, Mhe. Balozi Kombo ameelezea kusikitishwa na msiba huo na kueleza kuwa Papa Francis ataendelea kukumbukwa ulimwenguni kutokana na jitihada zake endelevu za kutetea haki, amani, maendeleo ya watu na ustawi wa jamii.
Naye Balozi wa Vatican nchini Askofu Mkuu Angelo Accattino amemshukuru Rais Samia na watu wote kwa salaam za rambirambi na faraja, huku akiwaomba Watanzania na mataifa kuendeleza utulivu na mshikamano katika kipindi hiki cha maombelezo, na kumuomba Mungu ampuzishe kwa amani Baba Mtakatifu Papa Francis.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news